YESU NAKUTUMAINIA

YESU NAKUTUMAINIA

Rosari ya Huruma ya Mungu

Tumia chembe za rozari ya kawaida

Baba yetu, uliye mbinguni Jina lako litukuzwe, ufalme wako ufike, utakalo lifanyike duniani kama mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku, utusamehe makosa yetu, kama nasi tunavyowasamehe waliotukosea. Usitutie kishawishini bali utuopoe maovuni. Amina.

Salam Maria, umejaa neema, Bwana yu nawe, umebarikiwa kuliko wanawake wote na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria mtakatifu mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.

Nasadiki kwa Mungu, Baba Mwenyezi, mwumba mbingu na dunia. Na kwa Yesu Kristu, Mwanaye wa pekee, Bwana wetu; aliyetungwa kwa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria, akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato, akasulubiwa, akafa, akazikwa, akashukia kuzimu; siku ya tatu akafufuka katika wafu; akapaa mbinguni; amekaa kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi; toka huko atakuja kuwahukumu wazima na wafu. Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Kanisa takatifu katoliki, ushirika wa Watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili, uzima wa milele. Amina.

Kila penye punje kubwa (Badala ya Baba yetu): Baba wa Milele, ninakutolea Mwili na Damu, Roho na Umungu, wa Mwanao Mpenzi sana, Bwana wetu Yesu Kristu, kwa ajili ya malipizi ya dhambi zetu, na dhambi za dunia nzima.

Kila penye punje ndogo (badala ya Salamu Maria): Kwa ajili ya mateso makali ya Bwana wetu Yesu Kristu, Utuhurumie sisi na dunia nzima.

Mwisho wa Rozari sali mara tatu sala ifuatayo: Mungu Mtakatifu, Mtakatifu mwenye Enzi, Mtakatifu unayeishi milele, Utuhurumie sisi na dunia nzima.

Rosari ya Huruma ya Mungu